Saturday, August 14, 2021

Ghafla - Koti Na Buti lyrics

Koti Na Buti

Ghafla

GENRE
Rap
Intro
Mtoto wangu analia peke yake barabarani analia barabarani mwenyewe
Mtoto wangu anasononeka
Lakini faraja yenu leo ni nguzo kwake
Hiki mlivompa
Arusha mbali ndugu zangu
Dar es salaam mbali

Chorus
Haikuwa pafyumu,ni jasho kali
Koti na buti kwa mguu sivui natanga mtaani
Vidonda vya tumbo,viliuma ndani
Kipindi sina chapaa na njaa ni kali
Haikua nafuu walaa hukujali
Ulisema usiogope komaa itakuwa afadhali

Verse 1
Napiga na simu kwa mama ikizidi hali
Jumlisha sijala mchana ila leo afadhali
Yote nawaza vipi nikupe mambo flani
Nikupe ile kitu unapaa fimbo ya mbali
Napanda nashuka napata nakosa naelea angani
Naona naibeba mitaa tunakwenda mbali
Kwenye hii safari ya mapito
Upendo unabebwa na mshiko
Usiende mbali na nilipo..Noo
Mbali sioni kabisa
Mbele naona kwa shida
Mboni yangu nakuita..Njoo
Fanya fasta ujongee
Fanya uje nipone
Fanya uje tuone..ooh
Natamani uone
Uishi ufarahie jioni
Tuliyochumia juani..Ooh

Chorus
Haikuwa pafyumu,ni jasho kali
Koti na buti kwa mguu sivui natanga mtaani
Vidonda vya tumbo,viliuma ndani
Kipindi sina chapaa na njaa ni kali
Haikua nafuu walaa hukujali
Ulisema usiogope komaa itakuwa afadhali

Verse 2
Huzuni furaha
Kulewa bar ni kwako
Najua sanaa
Uzuri wa mziki unao
Nimeumbiwa tamaa
Ninavyotamani unavyo
Silali kwa raha
Raha yangu unayo
Ningeweza vipi jiulize bila ya shabiki
Nitaishi vipi niulize bila ya rafiki
Rafiki yangu ni wewe mimi na mziki
Tumeishi sote kitambo bila ya usaliti
Wamekuja,wakaondoka
Nikaumia,nikasonga
Wakarudi,mmoja mmoja
Siwezi lipiza namuachia mola

Chorus
Haikuwa pafyumu,ni jasho kali
Koti na buti kwa mguu sivui natanga mtaani
Vidonda vya tumbo,viliuma ndani ndani
Kipindi sina chapaa na njaa ni kali
Haikua nafuu walaa hukujali
Ulisema usiogope komaa
Itakuwa afadhali
Haikuwa pafyumu ni jasho kalii
Vidonda vya tumbo
Koti na buti kwa mguu
Koti na buti kwa mguu sivui natanga mtaani
Koti na buti kwa mguu
Koti na buti kwa mguu sivui natanga mtaani

Related songs

XXKAXN JunkyardThe Pine TerçoTóy Tóy T-Rex По Едалу Замай и Слава КПСС Meet the fah Fah fah Gold diggersFamilyboso7 BurbsNanii2x Penny FarthingFAKE TYPE Die keys ​morten Ekspander eller dø Raga Rockers

No comments:

Post a Comment

宮野真守 - 1/13 lyrics

1/13 宮野真...